YANGA YATUA NUSU FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO
cha kikosi cha kocha Hans van der Pluijm cha Yanga leo kimefanikiwa kutinga nusu fainali ya michuano ya Kombe la FA, baada ya kupata ushindi wa mabao 2-1, dhidi ya Ndanda FC, ya Mtwara.
Ushindi wa leo ni ishara njema kwa Yanga ambayo inakabiliwa kucheza mechi nne katika siku 10 kuanzia leo ikijumuisha viporo vitatu vya mechi za Ligi ya Vodacom Tanzania Bara.
Katika pambano hilo lililopigwa uwanja wa taifa Dar es Salaam Ndanda ndio waliouanza kwa kasi mchezo huo wakiwa na matumaini makubwa ya kuitoa Yanga katika michuano hiyo inayofanyika kwa mara ya kwanza mwaka huu.
Quote " Ushindi wa leo ni ishara njema kwa Yanga ambayo inakabiliwa kucheza mechi nne katika siku 10 kuanzia leo ikijumuisha viporo vitatu vya mechi za Ligi ya Vodacom Tanzania Bara"
Mshambuliaji Atupele Green wa Ndanda, alifunga bao zuri dakika ya 6, lakini mshika kibendera Mohamed Mkono, alilikataa bao hilo akidai mfungaji alikuwa amezidi.
Yanga walijibu mapigo kwa kufanya shambulizi kali dakika ya nane lakini mshambuliaji wake Paul Nonga, alishindwa kuuweka mpira wavuni akiwa amebaki na kipa wa Ndanda FC Jeremia Kisubi, na shuti lake kupangliwa na kisha mabeki kuondosha mpira katika hatari.
Mchezo huo uliendelea kwa timu zote kushambuliana lakini Yanga ndio waliokuwa waliokuwa wameutawala zaidi mchezo na kutengeneza nafasi nyingi za mabao na dakika ya 27 Ngonga, aliweza kuifungia timu yake bao la kuongoza akiunganisha kwa kichwa mpira wa faulo uliopigwa na beki Juma Abduli.
Katika kipindi cha kwanza, Yanga waliweza kutengeneza nafasi nne za mabao lakini tatu walizipoteza mbili alipita Nonga na moja ilikuwa kwa Simon Msuva aliyegongesha mwamba wa juu na mpira kuokolewa na mabeki wa Ndanda FC.
Kipindi cha pili, Ndanda waliuanza mchezo kwa kasi na kuwasumbua vilivyo Yanga ambapo dakika ya 56 nahodha wake na mchezaji wa zamani wa Yanga Kigi Makasi, aliisawazishia Ndanda kwa bao safi lilitokana na mkwaju mkali ulioshinda kipa Deogratius Munishi ‘Dida’ na kuamsha nderemo kwa mashabiki wachache wa timu hiyo waliojitokeza uwanjani.
Kuingia kwa bao hilo kuliinzindua Yanga ambayo ilikuwa ikicheza bila nyota wake wawili wa kimataifa Haruna Niyonzima na Amissi Tambwe, na kuanza kufanya mashambulizi mengi kwenye lango la Ndanda lakini waliendelea kupoteza nafasi kupitia kwa Deusi Kaseke na Ngoma ambaye leo alikuwa amebanwa vilivyo na mabeki wa Ndanda.
Yanga waliendelea kuliandama lango la Ndanda na kufanya mashambulizi mengi ya hatari ambayo yaliweza kuzaa penati dakika ya 69, baada ya winga Simon Msuva kuangushwa ndani ya eneo la hatari na beki Paul Ngalema ambaye alitolewa nje kwa kadi nyekundu na mwamuzi Jimmy Fanuel, na beki Kelvini Yondani aliitumia vizuri nafasi hiyo kwa kufunga bao la pili lililoivusha timu yake hadi nusu fainali na kuwatoa Ndanda walioshinda mechi mbili za mwanzo kabla ya huo.
Yanga iliendelea kuutawala mchezo na kufanya mashambulizi mengi kweye lango la Ndanda na kuendelea kupoteza nafasi nyingi ambazo walizipata.
Mshambulaiji wa Ndanda Omary Mponda, alipata nafasi ya wazi dakika ya 81, lakini shuti lake alilopiga halikuweza kulenga bao na kupaa juu na kuwa faida kwa Yanga.
Katika dakika ya 84, nahodha wa Yanga aliyekuwepo nje kwa muda mrefu Nadiri Haroub ‘Cannavaro’ aliingia uwanjani kuchukua nafasi ya Kelvin Yondano na kuonyesha kiwango cha juu ikiwa ni mchezo yake ya kwanza tangu alipopona majeruhi yake.
Ushindi wa leo Yanga imekungana na Mwadui FC, iliyokuwa ya kwanza kutinga hatua hiyo baada ya kuifunga Geita Goal Mine.

Comments
Post a Comment