WILSHERE, CECH WAREJEA RASMI MAZOEZINI

Kiungo wa Arsenal Jack Wilshere amerejea kwa mara ya kwanza mazoezini baada ya kuumia kwa zaidi ya takribani miezi 9. kiungo huyo ambaye anasumbuliwa na tatizo la kifundo cha mguu anategemea kukaa benchi wakati ti mu ya ke ya Arsenal ikimenyana na Watford hapo kesho April mbili katika uwanja wa emirates.
kocha Arsene Wenger amesema kwamba Jack anatarajiwa kuwepo katika benchi hiyo kesho
Quote " Jack amerudi na natarajia kuitwa katika kikosi cha England kwa ajili ya michuano ya ulaya, nina furaha na maendeleo yake na anatarajia kuwa fiti zaidi ili kumaliza michezo yote ya ligi kwa ajili ya kuisaidia Arsenal"
Wenger pia amedokeza kuwa kipa Petr cech atakuwepo katika mechi ya kesho baada ya kupona maumivu yaliyokuwa yakimsumbua kwa muda wa mwezi mmoja


Comments
Post a Comment