PARLOUR : NI MUDA WA WILSHERE KUONYESHA KILE ALICHONACHO

Time for Wilshere to get fit and off the front pages, says Parlour

Kiungo wa zamani wa arsenal Ray parlour amemtaka jack wilshere kuonyesha kiwango cha juu baada ya mchezaji huyo wa Arsenal kupona majeraha yaliyomsumbua ndani ya miezi tisa. wilshere hajafanikiwa kucheza mechi yoyote ya arsenal msimuu huu jambo ambalo parlour amemsisitiza kuonyesha nini alichonacho katika kuelekea michuano ya Ulaya 2016 itakayofanyika ufaransa ambayo jack wilshere ana nafasi kubwa ya kuitwa endapo atafanikiwa kufanya vizuri katika mechi 7 zilizobaki za ligi kuu ya England.
   Parlour akiongea na Betfair Lalisema "wilshere ni mchezaji mzuri sana,muangalie akiwa amevaa jezi ya timu ya taifa ya Uingereza chini ya Roy Hodson anacheza vizuri sana"
              " ana nafasi kubwa ya kucheza ndani ya arsenal na England kwa kuwa ana uwezo wa kucheza katika nafasi nyingi za kiungo wa kati lakini anatakiwa awe fiti muda wote na hicho ndicho kitakachomsaidia yeye kucheza katika kiwango cha juu"

            "amekuwa akiumia sana ndani ya misimu miwili, mitatu na hiyo ina athiri sana muda wake katika soka, hivyo nategemea kwa sasa akiwa fiti afanye mazoezi yatakayo muwezesha yeye kucheza katika kiwango kinachotakiwa"

Pia Parlour aliongelea kuhusu Wilshere anavyoandamwa na vyombo vya habari kutokana na tabia yake nje ya uwanja. Alisema
          " Ukiangalia katika kurasa nyingi za magazeti, jack yupo katika kurasa ya mbele, hicho siyo kitu kizuri sana kwake kama mchezaji. Anatakiwa kuwepo katika kurasa za nyuma za magazeti, kitu tunachotegemea ni yeye kurudi katika kikosi ili kujiandaa vema na michuano ya EURO".

Arsenal wanatarajia kukutana na west ham hapo kesho katika uwanja wa upton Park, katika mechi itakayopigwa majira ya saa tisa jioni kwa saa za afrika mashariki.

Comments