DARMIAN AITAKA UNITED KUCHEZA UEFA MSIMU UJAO

Darmian: Man Utd must secure top-four finish

Beki wa kulia wa manchester united mateo darmian ameitaka timu yake ya manchester united pamoja na wachezaji wenzake kuhakikisha wanafanya kila mbinu ili timu hiyo iweze kushiriki michuano ya Ulaya Msimu ujao. Timu hiyo ya mashetani wekundu itakuwa na kibarua kigumu cha kuifunga tottenham hotspurs hapo jumapilii ili kuendelea na mbio zao za kuhakikisha wanaingia top four ya Uingereza. Man United pia watakuwa wanaiombea arsenal kuifunga west ham hapo kesho ili kupunguza kasi ya vijana hao wa Bilic ambao ni washindani wa manchester united katika mbio za top four. Timu nyingine itakayokuwa ikiangaliwa zaidi na manchester united itakuwa ni man city ambao pia ni washindani wa united katika mbio za top four, City watacheza mechi yao kesho jumamosi dhidi ya westbrom.

 Katika hatua nyingine kiungo wa man united Marouane Fellaini ameionya tottenham na kusema kwamba kikosi chao kina uwezo wa kuifunga timu yoyote ile itakayokabiliana mbele yao.
 Fellaini alisema
             " ni mechi nzuri na yenye mvuto wa aina yake lakini tuna uhakika timu yetu itashinda na tutafanya kila linalowezekana ili tuweze kucheza michuano ya ulaya msimu ujao.
Fellaini warns Tottenham: Man Utd have the quality to beat anyone
Marouane fellaini

Comments