HARRY KANE MCHEZAJI BORA WA MWEZI EPL

Kane named Player of the Month as Ranieri scoops manager award
Harry Kane


Mshambuliaji wa Tottenham Harry kane ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi  EPL baada ya kufunga magoli matano ndani ya mwezi march na kuisaidia timu yake kuendelea na mbio za ubingwa wa uingereza msimu huu. Mabao ya Kane aliyafunga dhidi ya arsenal ambapo alifunga goli moja katika sare ya 2-2, mabao mengine manne aliyafunga dhidi ya aston villa na bournemouth ambapo katika kila mechi alifunga magoli mawili.

           Kwingineko Kocha wa Vinara wa ligi hiyo ya EPL Muitaliano Claudio Ranieri ametwaa tuzo ya kocha bora wa mwezi march baada ya timu yake kufanya vizuri katika mwezi march kwa kupata pointi 10 kati ya 12 ndani ya michezo minne, leicester itakutana na sunderland hapo kesho ili kujaribu kuendeleza rekodi yao hiyo ya ushindi katika mbio za kulisaka taji la EPL Msimu huu.

Comments