KIKOSI CHA MANCHESTER UNITED -21 CHATANGAZWA MABINGWA WA ENGLAND

Man Utd Under-21s win Premier League title

Wakati mholanzi Louis Van Gaal akihangaika na akina Wayne Rooney katika kukimbizana na mikiki mikiki ya ligi kuu ya England, Juzi kikosi cha Manchester United chini ya umri wa miaka 21 kilitawazwa mabingwa wa england kwa mara ya tatu ndani ya miaka minne na kuandika historia katika ligi hiyo. vijana hao wakiongozwa na baadhi ya wachezaji wanaopata uzoefu katika kikosi cha kwanza kama Guillermo Varela na Andreas Perreira walitangazwa mabingwa baada ya kuifunga Tottenham Hotspurs 3-2 katika uwanja wao wa White hart Lane. mabao ya united -21 yalipatikana kupitia Andres Perreira, Guillermo Varela na Donald Love.

Kikosi hicho kipo chini ya kocha Warren Joyce kimefanya hivyo mara ya Pili mfululizo baada ya msimu wa mwaka jana kuwa mabingwa wa ligi hiyo ya chini ya umri wa miaka 21.

Comments