AGUERO AFIKISHA KARNE MOJA UINGEREZA

Mu Argentina Sergio Kun Aguero Juzi alifikisha mabao 100 katika Ligi kuu ya England na kuwa mchezaji wa pili nyuma ya Alan Shearer kwa kufikisha idadi hiyo kutokana na mechi alizocheza. Bao alilofunga juzi katika mchezo dhidi ya kikosi cha Rafael Benitez ambao uliisha kwa sare ya bao 1-1 lilimfanya yeye kuwa moja kati ya wachezaji 25 katika historia ya ligi kuu ya England kufikisha mabao 100. Hat trick aliyopiga dhidi ya Chelsea hapo jumapili ilipelekea yeye kuwa na mabao 99 katika mechi 146 katika ligi hiyo. Bao lake lake hilo dhidi ya newcastle lilimfanya yeye kuandika rekodi hiyo ya kuwa moja katika ya wachezaji waliofikisha mabao 100 katika ligi ya England.

Comments
Post a Comment