MAONI: JINSI REAL MADRID ATAKAVYOMTOA WOLFSBURG ROBO FAINALI

Pamoja na kufungwa magoli 2-0 wakiwa ugenini dhidi ya Wolfsburg ya Ujerumani, Ninaamini Timu ya Real madrid ina uwezo mkubwa wa kupenya robo fainali kwa asilimia zaidi ya 60%... Zifuatazo ni sababu za maoni yangu kwamba ni kivipi timu ya real madrid inaweza kuifunga Wolfsburg na kuingia katika hatua ya nusu fainali.
1. UWIANO MZURI WA MAGOLI KATIKA MECHI ZA NYUMBANI
ukiangalia katika misimu mingi ya hivi karibuni timu ya Real madrid imekuwa na uwiano mzuri wa magoli katika ligi ya hispania na katika mashindano yote kwa ujumla hasa katika uwanja wao wa nyumbani Santiago Benarbeu, msimu huu real madrid wana advantage ya magoli 64 katika ligi japo wanashika nafasi ya tatu, timu inayoongoza ligi hiyo FC Barcelona ina magoli 60 na atletico madrid inayoshika nafasi ya pili yenyewe ina magoli 38. katika uwanja wao wa bernabeu wana uwiano wa kufunga magoli Matatu hadi manne ndani ya mechi moja katika msimu huu, naamini uwiano huu utaisaidia sana real madrid katika kutafuta nafasi yao ya kuingia nusu fainali.
2. TEAM WORK
Kocha wa real madrid Zidane amesema kuwa hawatokubali kucheza tuu ili kupata matokeo, badala yake watacheza kama timu kwa kutomuangalia mchezaji mmoja mmoja, hii inakuja pale ambapo katika mechi ya kwanza Wachezaji nyota wa real madrid, Ronaldo, Bale, na Benzema walishindwa kuonyesha makali yao katika lango la wolfsburg na kufanya timu yote na wachezaji wa nafasi nyingine kupata wakati mgumu wa kushambulia baada ya kuona fowadi zao ni butu mbele ya lango. Kutegemea uwezo wa mchezaji mmoja mmoja unaweza ukakusaidia ila katika mechi kama hii lakini kitu kinachohitajika ni timu kucheza kama timu ili kuhakikisha kila mmoja anakuwa na uwezo wa kujiamini mwenyewe.
3. MORALI YA KUTAFUTA USHINDI
Kitu kingine kitakachoisaidia real madrid ni wachezaji kuwa na morali ya ushindi kutokana kwamba wao ndio wapo nyuma kwa goli mbili. hivyo wanatakiwa kufanya kila mbinu ili kuhakikisha wanapata matokeo ya kuridhisha kwa kucheza kwa kujituma na kwa kiwango cha hali ya juu ukizingatia wolfsburg watakuja na mbinu za kuwaharibia real madrid ili wakose kujiamini na kuharibu morali ya mchezo kwa wachezaji wa real madrid.
4. ENEO LA ULINZI
Katika eneo la ulinzi timu zote zipo vizuri kama wofsburg wana mabeki kama Bonifem Dante na Naldo ( wote raia wa brazil) ambao ni mabeki wazoefu na wanaoweza kuzuia mashambulizi kwa kushirikiana kama walivyofanya katika mechi ya kwanza. kwa upande wa real mmadrid Beki mbrazili Marcelo amekuwa na msimu mzuri sana na real madrid, amekuwa anacheza kwa kujiamini na kusaidia timu kupandisha mashambulizi akitokea upande wa kushoto. Beki mwingine anayetazamiwa kulinda ukuta wa real madrid ni Sergio Ramos ambaye atakuwa na kibarua kizito cha kukabiliana na kipaji cha Wolfsburg mjerumani Julian Draxler ambaye ameng'ara sana na wolfsburg msimu huu akitokea Schalke 04 ya ujerumani, na kuwa nguzo ya vigogo hao wa VOLKSWAGEN.
Top Betting
Real Madrid 4-1 Wolfsburg
Real Madrid 3-0 Wolfsburg
Real Madrid 4-0 Wolfsburg.

Comments
Post a Comment