Skip to main content
FORLAN AMPIGIA CHAPUO MOURIHNO KUTUA MAN U
 |
| Jose Mourihno |
Mchezaji wa zamani wa Manchester United na Timu ya taifa ya Uruguay Diego Forlan, Amempigia chapuo kocha mreno mwenye maneno mengi Jose Mourihno. forlan ambaye amecheza chini ya kocha Alex ferguson alikaririwa na 888.com alisema
"nadhani kitu wanachokipitia manchester united kwa miaka miwili sasa kinaweza kutatuliwa na mourihno"
Jose mourihno amekuwa akitajwa kama mrithi wa kocha wa sasa wa united mholanzi Louis Van gaal huku pia akiendelea kupingwa na baadhi ya ma lengendari wa united na viongozi wengine kama sir Alex Ferguson na Paul Scholes. Forlan aliongelea swala la Giggs kupewa Timu lakini akatoa maoni yake akisema kwamba giggs bado hajapata uzoefu wa kutosha wa kuifundisha united.
 |
| Diego Forlan |
Comments
Post a Comment