KAMA POGBA MAN U, CHELSEA WAJUTIA KWA DE BRUYNE
![]() |
| De Bruyne akiwa katika uzi wa City |
Kocha wa City Manuel Pellegrin amesema klabu ya Chelsea hawana budi kujutia kuuzwa kwa Kevin De Bruyne kama ilivyo kwa Manchester United wanavyojutia kwa kuuachia Paul Pogba kwa uhamisho wa bure kwenda Juve. Viungo hao wawili wanaokipiga katika vilabu viwili tofauti wamekuwa lulu inayotamaniwa sana na vilabu vingi katika soka la Ulaya, juzi De Bruyne alifunga bao dhidi ya Psg lililoiwezesha City kupita katika hatua ya Nusu fainali kwa mara yao ya kwanza Tangu kuanzishwa kwa michuano hiyo. wengi tunadhani angekuwa ndiye mchezaji bora wa Epl msimu huu kama asingepatwa na majeraha yaliyomkuta mwezi februari na kupelekea kukaa nje kwa miezi miwili.
Pellegrin alisema :
" akiwa chelsea alikuwa bado mdogo, jina lake halikutajwa na watu wengi kama sasa na ilikuwa ni vigumu kwa yeye kucheza mbele ya majina makubwa yaliyokuwa pale chelsea kipindi na yeye pia akiwa ni mchezaji, hiyo inatokea kwa timu nyingi. Kikubwa ni kwa yeye kwenda Ujerumani ili kuongeza uzoefu uliomfikisha hapa, natumaini ataendelea kuwa mchezaji muhimu sana ndani ya city kwa miaka ijayo"
De Bruyne aliondoka Chelsea 2014 baada ya kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza na kutimkia Ujerumani katika klabu ya Wolfsburg na kuwa mchezaji muhimu katika kikosi hicho akisaidia kutengeneza nafasi nyingi zaidi za magoli ulaya kwa msimu uliopita kwa kuiwezesha klabu hiyo kushiriki michuano ya Ulaya msimu huu, baada ya hapo City walitoa Paundi 54 millioni na kunasa saini yake na kmleta katika ligi kuu ya Uingereza na kuendeleza moto wake kwa kuipatia mafanikio City kwa msimu huu.


Comments
Post a Comment