BARCELONA NJE YA MICHUANO YA ULAYA: NINI HASA CHANZO CHA KUTOLEWA

Messi on worst scoring run in six years

Jana Usiku timu ya Fc Barcelona ilitolewa nje ya michuano ya Ulaya na klabu ya Atletico Madrid kwa kufungwa mabao 2-0, niliona jinsi atletico madrid walivyocheza kwa kujua ni nini hasa wanakihitaji katika mechi hiyo. Akilini mwao walikuwa wanajua wanahitaji goli moja tuu ama zaidi bila kuruhusu goli kutoka kwa Barca ambalo lingeweza kuwaondoa Barcelona kwenye michuano hiyo, kulikuwa na wachezaji wa 3 kama sio wa 4 ambao uwezo wao ungeweza kuwasumbua Fc Barcelona mmoja wao ni huyu mfaransa Antoine Griezman; ana akili sana ya soka, hana nguvu ila spidi yake akiwa na mpira inatisha, anajua kufunga anatoa pasi za mwisho na kikubwa zaidi ni ule mguu wake wa kushoto ambao nadhani kwa msimu ujao vilabu vingi vikubwa vitatenga kiasi kikubwa cha fedha ili kuupata. kwa maoni yangu binafsi kuna vitu nilivyoviona ambavyo viliifanya Barcelona kushindwa kwenda na Spidi ya vijana hao wa Simeone na kujikuta wameangukia pua mwisho wa mechi hiyo.

1. KUJIPA UHAKIKI WA KUPITA
Hiki kitu kilifikiriwa na watu wengi sana ambao ni wapenzi wa Barcelona na mashabiki wengine wa mpira wa miguu, nadhani hata wachezaji wa Barca walicheza huku vichwani mwao wakijua kwamba fainali itakayopigwa pale Milano mwezi Mei itakuwa ni wao dhidi ya Real Madrid Au Bayern Munich, kujipa uhakiki huu ni kitu ambacho kiliwaathiri kiakili na hasa baada ya kuona mambo yanaenda ndivyo sivyo kati kati ya mechi ambapo walishindwa kuupata mchezo wa atletico madrid na kujikuta kwamba wao wana kazi kubwa ya kutafuta ushindi zaidi ya Atletico ambao ndio walikuwa nyuma kwa mabao mawili dhidi ya moja. Kitu muhimu hapa ni kuwapa sifa Atletico madrid maana wao walicheza na akili za wachezaji wa Barca kwa kuhakikisha kuwa fikra walizonazo juu yao na mawazo ya mashabiki wengi yalikuwa ni ya kuwapa moyo tuu Barcelona.

2. SAFU MBOVU YA ULINZI
Baada ya Griezman kuipatia Atletico bao la kwanza nilikumbuka fainali ya 2009 Pale jiji la Roma Italia ambapo Lionel Messi alifungwa bao la kichwa dhidi ya Manchester United akiwa kati kati ya mabeki Rio Ferdinand na Nemanja Vidic wenye Urefu wa Futi 6 na point kadhaa, tuyaache hayo. Griezman ana urefu wa Futi 5.8, Gerald Pique ana urefu wa Futi 6.4 na Javier Mascherano an urefu wa futi 6.0, kwa akili ya kawaida mtu kama Griezman huwezi ukategemea anaweza kuruka juu zaidi ya Pique au Mascherano lakini katika mechi ya jana mfaransa huyo alifunga goli la kichwa akiwa analindwa na beki Gerald Pique. ubovu wa safu ya ulinzi ya Barcelona ulionekana dhahiri katika mechi hiyo na hata katika goli la pili unaona Phelipe luis anakokota mpira kuanzia nusu ya uwanja akiwa hana mtu anayemkaba mpaka anaingia ndani ya boksi na kusababisha penalty, safu ya barca ilionyesha mapungufu sana katika magoli yote ya jana na pia katika mechi nzima.

3. UTEGEMEZI WA WACHEZAJI
Kila mtu akiiongelea Barca atakwambia kuhusu Neyma, Suarez au Messi, utamaduni huo umejengeka hata ndani ya Barcelona,ni vizuri kuwa na wachezaji kama hawa ambao wanaweza wakabadilisha matokeo katika mechi, lakini katika mechi kama ya jana ilipaswa kila mchezaji acheze kwa kuangalia timu inahitaji nini zaidi ya kuangalia timu inamuhitaji nani, lakini kwa kuwa wachezaji wengine wameathiriwa kiakili kuwa MSN wapo mbele hivyo mambo yataenda sawa ndiyo maana saa nyingine wanasahau majukumu yao, mfano mzuri ni kwamba watatu hao msimu uliopita walifunga magoli 122 peke yao huku timu nzima ikiwa na mabao 137 ina maana kwamba wachezaji wengine walifunga magoli 15 tuu ndani ya msimu mzima, hii haileti maana yeyote kwenye Team Work. na hiki kitu kiliwa gharimu sana katika mechi ya jana.

4.KUSHUKA KWA FORM YA MESSI
Hii ni madhara ya kitu kilichoongelewa kuhusu utegemezi wa wachezaji, kwa sasa Messi ndiye mchezaji muhimu zaidi katika kikosi cha Barcelona, lakiki ndani ya dakika 452 ameshindwa kufunga bao lolote katika mechi zilizopita, mara ya mwisho ilikuwa 2010, jana alishindwa kupiga shuti lolote lililolenga golini, mara ya mwisho ilikuwa 2014 pia dhidi ya Atletico Madrid ( tuwaite tuu wahuni wa jiji la Madrid). Hii inaiathiri saba Barcelona maana katika mechi kama hii ya jana ilihitaji sana mchezaji kama Messi awe kwenye Form ya hali juu ili kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa uwanjani lakini kwa jana ilishindikana kabisa maana kila mtu anamuangalia yeye, kushindwa kupiga hata shuti moja langoni haileti maana sana kama mchezaji bora wa Dunia ambaye unategemea kuisaidia timu yako kubeba kombe hilo la Thamani zaidi Barani Ulaya.
Ancelotti: Why Barcelona failed
wachezaji wa Barca wakimlalamikia mwamuzi baada ya kiungo wa Atletico Madrid Gabi kunawa mpira katika eneo la Hatari.

Hakuna budi kuwapongeza Atletico Madrid kwa kazi wa liyoifanya Jana na kuipongeza kila timu iliyofanikisha kuingia katika hatua ngumu zaidi ya nusu fainali ambapo kila mtu atacheza ili kuhakikisa mwezi mei pale milano patamuhusu.
Griez lightning! Barca treble hopes end
wachezaji wa Atletico wakishangilia Baaya kupata ushindi uliowapa tiketi ya kucheza nusu fainali

Katika matokeo mengine pia tulishuhudia Klabu ya Bayern Munchen ya Ujerumani ikikata tiketi ya kuingia nusu fainali baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Benfica ya Ureno. Mabao ya Bayern yalifungwa na Artro Vidal na Thomas Muller huku yale ya Benfica yakifungwa na Jimenez na Tallisca. pongezi kwa vija na wa Pep Guardiola.
Vote for the UCL Goal of the Week
Arturo Vidal akishangilia baada ya kufunga goli dhidi ya Benfica
Kichombezo " Timu zote zilizopita katika hatua ya Robo fainali zimepita kwa Aggrigate ya mabao 3-2"
ROBO FAINALI
Real Madrid            3 - 2     Wolfsburg
Bayern Munchen     3 - 2     Benfica
Man city                  3 - 2      PSG
Atletico Madrid       3 - 2      Barcelona

Comments